UNAWEZAJE KUPATA WAZO LA BIASHARA?
Sehemu ya nne.
Namna ya pili ya kupata wazo la biashara.
Kutokea ndani. Hii ni namna ya kufikiri kama mgunduzi au mwasisi wa wazo. Hii ni namna inayokupa kufikiri kutoka 0 kwenda 1. Tofauti na jinsi nyingine ambazo huwa mwendelezo wa kutoka moja hadi hatua nyingine.
Aina hii ya kufikiri huja kwa watu ambao kwa makusudi huamua kuja na ufumbuzi mpya kwa tatizo au kwa watu ambao kwa kukusudia huamua kutengeneza tatizo na kisha wao kuwa na ufumbuzi wa tatizo.
Suala la mhimu hapa kuelewa ni kuwa hakuna biashara ambayo inazaliwa nje ya muktadha wa changamoto ambazo zinatuzunguka, ikiwa unaweza kutoa suluhisho kwa changamoto yoyote iliyopo basi watu watakuwa radhi kuipa thamani ya kifedha.
Pamoja na kuwa namna hii ya kufikiri hutokea ndani, motisha kuu ya kufikiri hivi hutokea nje na mara nyingi Inaweza kuwa kutaka hali ya mtu iliyopo, kupata heshima au kupata utajiri.
Namna hii ya kufikiri ina gharama zake ukilinganisha na namna ya awali ya kufikiri kwa sababu mara nyingi inahitaji nguvu kubwa ya kuanza wazo lako sababu ya ukinzani uliopo kama kukataliwa kwa wazo lako, kuvunjwa moyo, na bidhaa au huduma yako kukosa wanunuzi. Lakini changamoto kubwa huchagizwa na kuwepo kwa uzito wa watu kupokea mambo mapya.
Kanuni za msingi kufikiri kwa namna hii.
1. Elewa kuwa bado kuna mambo mapya mengi ambayo hayajagunduliwa hata leo. Bado unaweza kuja na wazo jipya.
2. Tafakari ni tabia ya mhimu katika ugunduzi.
3. Udadisi na uwezo wa kuuliza kwanini kwa vipi ni nyenzo mhimu ili kugundua.
4. Elimu si ile tunapokea ni kile tunachoweza kutoa kama matokeo ya vile tulivyopokea.
5. Wewe ni mtu tofauti na kwa sababu hiyo una kusudi maalum katika maisha haya (special mission).
6. Fursa zina tabia za kuzaana, fursa moja hutengeneza fursa ya pili.
7. Wazo kuwa jema si lazima likubalike na watu wote.
Nieleze kwa kiasi siku za leo tunafurahia mawasiliano ya Internet katika computer zetu na simu lakini inawezekana kabisa aliyegundua wazo la kuwa na computer hakufikiri kuwa na wazo la kuwa na Internet na computer ilifanya kazi kama mashine moja tu yaani kama mithili ya kikokotozi.
Bill Gates alipata wazo la kuanza kuwa na software kwa sababu computers zilikuwepo na si yeye mgunduzi wa computer lakini kwa kuangalia na kujifunza sana namna computer ilifanya kazi aliona kuna pengo na yeye akathubutu kuli ziba.
Kabla ya kuanza kuwepo mitandao ya kijamii kulikuwapo na Google ambao namna yao ya kufanya kazi haipo sawa sana na jinsi Facebook wanafanya kazi hali kadharika mitandao mingi ya kijamii iliyopo.
Nataka uondokane na dhana kwamba hakuna kitu kipya unaweza kugundua, ugunduzi ni wazo lakini badaye hilo wazo hufanyiwa kazi ili lipate picha yake kamili.
Ni nani anayeweza kugundua?
Ni profesa, mwanasayansi, msomi au mtu yoyote wa kawaida?
Watu ambao waligundua na kurusha ndege kwa mara ya kwanza waliambiwa na profesa wa hesabu haliwezekani kulusha kitu angani lakini waliendelea mbele kwenda kulusha ndege yao ya kwanza.
Phillip Shijanga kijana Mtanzania siku chache zilizopita alikuja na kiti cha wagonjwa kinachoweza kujiendesha, kugeuka kuwa kitanda na kinachoweza kuendeshwa kwa sauti (imla). Alikuwa na wazo, akalitafsiri katika mchoro na badaye akatumia malighali kuliumba au hata watu wengine wangeweza kwa kufuata ule mchoro.
Changamoto kubwa ambayo tunapata ni kuwa tunapopata wazo ambalo huonekana si kawaida mara nyingi hatulipi nafasi, na hata kama likiwapo hatulifanyi liishi na kuweza kulitafsiri katika maandishi au mchoro ili liweze kupata maana yake na pia hatuwezi kulipa muda wa kukomaa. Kimsingi hatukai katika wazo moja kwa muda.
Rafiki yangu Justine alikuwa na wazo la k
Watu wengi tunahamasika kwa muda lakini ile hamasa inapo koma tunaamua kuacha na kurudia tulipo paacha tunashindwa kukaa na hamasa kwa muda mrefu juu ya jambo moja tunalo lifanya.
Kama ambavyo mabinti wengi wanatoa mimba, kadharika mawazo mengi hayapati hata nafasi ya kuona jua au kuishi kwa siku moja. Mimba za mawazo mazuri ambayo yamekufa ni nyingi kuliko mimba za watoto. Laiti kama mawazo haya yangetokea hata siku moja inawezekana yangeishi miaka elfu..
Hebu fikiri kama wagunduzi wa ndege wangetoa mimba ya wazo la kuwa na usafiri wa anga, fikiri kama Edson angefikiri kutoa mimba ya kutengeneza gari, fikiri kama Shigongo angeamua kutoa mimba ya Global publishers, fikiri kama ningetoa mimba ya andiko hili??
Laiti kama Mungu angetupa tathmini ya kuelewa ni kiasi gani sisi ni sababu ya kuwa hapa tulipo, tungelaani kwa nini tuliamua kutoa zile mimba..
Stop Ideas Abortion..
BIG RESULTS NOW


